Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II TGS B (27)

at Judiciary of Tanzania
Location Dar es salaam, Tanzania, United Republic of
Date Posted May 7, 2020
Category Legal
Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

Overview

The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 vests the authority and responsibility to administer justice in the Judiciary of Tanzania. The Judiciary has its foundation on Article 107A (1) and 107B of the Constitution and states clearly about the Independence of the Judiciary in the United Republic of Tanzania. Now the strategic plan for Judicial Independence is focused in both form and content.


1:2 Mandate of Judiciary
The mandate of Judiciary to perform its functions is obtained from the Constitution of the United Republic of Tanzania vide article 107 and its primary function is to dispense justice with equity and compassion according to laws of Tanzania.

JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
UMOJA NA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 195
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine, mamlaka ya kuajiri watumishi wa Mahakama wa kada mbalimbali.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania kwenye Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi..

Kazi za kufanya:
• Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajika na wasomaji.
• Kudhibiti upokeaji, uandikishaji kumbukumbu/nyaraka.
• Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka Katia reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
• Kunukuu (kurekodi) mwenendo mzima wa kesi na kuweka kumbukumbu sahihi za mashauri yanayosikilizwa na Majaji au Mahakimu.
• Kuhakiki na kuandaa taarifa iliyohakikiwa na kuwasilisha sehemu husika kabla yakutoa nakala kwa Umma.
• Kufanya kazi nyingine za kiutawala zinazohusu masuala ya kimahakama kama kuwasilisha nyaraka za kisheria Mahakamani na kuangalia muda na siku ya kufanyika kwa kesi husika.
• Kuthibitisha machapisho (transcripts) kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi ndani ya muda uliopangwa.
• Kutunza na kuhifadhi machapisho (transcripts) mahali salama.
• Kuratibu utoaji wa machapisho (transcripts).
• Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa.

Job Skills: Not Specified

Sifa za Kuingilia:
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti/Stashahada ya utunzaji kumbukumbu kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma pamoja na wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Diploma ya Sheria kutoka chuo cha Uongozi wa Mahakama.

Applying Instructions

Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 21/05/2020 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:

  •  Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo. - Wasifu wa mwombaji (CV).
  • Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  • Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni ambazo zimeandikwa majina nyuma yake .
  • NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/ sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).

Aidha, inasisitizwa kwamba:

  •  Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44
  • Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa Wilaya anayoishi mwombaji.
  •  Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.
  •  Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
  •  Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
  •  Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.
  • Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
  • Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.
  •  Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.
  •  Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.
  •  Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391, DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;
Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391, DAR ES SALAAM,