Kwa GHARAMA NAFUU Kabisa, Tunakupa Ushauri Wa Kitaalamu wa Jinsi ya Kupata KAZI

at Business Consultancy Services
Location Dar es Salaam, Tanzania, United Republic of
Date Posted June 24, 2021
Category Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

Description

ANGALIZO.

Kwanza kabisa, ieleweke wazi kabisa huduma hii SI BURE! Ni huduma ya kulipia. Hata hivyo habari njema ni kuwa Gharama yake ni Nafuu sana.

JINSI YA KUWASILIANA NASI

Ili kuwasiliana nasi, tazama upande wa mkono wa kulia wa tangazo hili. Utaona alama ya Simu. Soma maelekezo yaliyoandikwa chini ya hiyo alama ya simu.

Hebu tafadhali usimalize kusoma tangazo hili na kuondoka tu. Hakikisha unatuma ujumbe mfupi kwetu wa kuulizia gharama za huduma hii. Nasi tutawasiliana nawe na kukuelezea gharama zetu.

ZINGATIA

Ili ufaidike na huduma yetu soma tangazo hili lote kwa utulivu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Tangazo hili limeandikwa kwa Kiswahili na kwa Kiingereza. Ukilisoma katika lugha mojawapo utakuwa umepata ujumbe wote uliokusudiwa.

Kimsingi, huduma tunayoitoa ni ushauri wa kitaalamu TU! Yaani Business Consultancy Services. Na ieleweke vema kuwa sisi Hatutoi Ajira. Yaani sisi si Waajiri. Wala hatuwashawishi waajiri ili watoe upendeleo wa ajira kwa watu fulani. LA HASHA!

Iwapo utaamua kutumia huduma yetu, tunachokifanya ni kushirikiana na wewe kuandika kitaalamu nyaraka za maombi ya kazi. Sasa, huo utaalamu wa kuandika maombi ya kazi, ndiyo eneo letu bobezi. Na hiyo ndiyo huduma yetu. Yaani maombi yako yatoe taswira halisi ya elimu, mafunzo, ujuzi na uzoefu ulionao. Imani yetu ni kuwa ubora wa nyaraka zako utawasababisha waajiri watamani kukuona ana kwa ana ili uwathibitishie kile walichokiona katika maandishi. Lakini wajibu wa mwisho ni wa kwako na wewe mwenyewe ndiye utakayefanya uhariri wa mwisho na kuhakikisha kuwa kila kilichoandikwa ni sahihi. Pia, ni wewe mwenyewe ndiye utakayetuma maombi kwenda kwa waajiri na kuhusika na chochote kitakachoendelea baada ya hapo.

Sasa, kama umevutiwa na utangulizi huo hapo juu, endelea kusoma maelezo ya ziada hapa chini. Utagundua kuwa msaada wa kitaalamu ni wa muhimu sana kwani ni ujuzi wa kipekee.

MSAADA WA KUANDIKIWA MAOMBI YA KAZI KITAALAMU

Je, bado hujapata KAZI? Je, umehitimu elimu ya Diploma au zaidi kutoka mojawapo ya Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Elimu ya Kati, Vyuo vya Ufundi Stadi (mfano VETA), n.k.? Kama jibu lako ni NDIYO, basi karibu tukusaidie.

Je, ungependa kusaidiwa kuelekezwa jinsi ya kuandika kitaalamu nyaraka zako za maombi ya kazi (yaani, WASIFU wako, BARUA zako, n.k.) kiasi kwamba zitaacha taswira ya kuvutia na isiyofutika akilini mwa msomaji yeyote yule na hasa mwajiri unayemlenga? Kama jibu lako ni ndiyo, basi huduma yetu itakufaa.

Lakini awali ya yote, hebu tuelezane ukweli: hapa Tanzania, kwa kila tangazo moja la nafasi ya kazi (hasa katika sekta binafsi), waajiri hupokea takribani nyaraka 1000 hivi kutoka kwa wanaotafuta kazi. Katika hali kama hii si ajabu kwamba hakuna muda wa kutosha kuzitazama kwa muda mrefu nyaraka za kila mwombaji. Ni wastani wa sekunde zisizozidi 10 hutumiwa kupitia nyaraka za kila mwombaji. Katika hatua hii maombi mengi hutupiliwa mbali na machache tu ndiyo huendelea kusomwa kwa kina zaidi. Na hata kama zingetazamwa kwa muda mrefu, haibadilishi kitu: ya kwamba nafasi inayogombaniwa ni moja au chache na waombaji ni wengi! Kwa vyovyote vile katika hatua hii wengi wataachwa tu. Suala hapa ni je, wewe utakuwa miongoni mwa hao wachache watakaopenya kwa hatua inayofuata? Kwa bahati mbaya katika hatua hii ni nyaraka zako tu ndizo zinazokuwakilisha. Wewe mwenyewe bado haujaitwa wakati huu. Bila shaka kila mtu anatamani kwamba angewakilishwa na nyaraka ambazo zitampa nafasi ya kuitwa na hatua inayofuata ya usaili au mahojiano.

Ni kwa msingi huu, ili upenye katika hatua hii ni lazima maombi yako ya kazi yawe yamepangiliwa kweli. Yawasilishe fikra pevu, yawaaminishe wachambuzi kwa hoja nzito za kitaalamu na kuoanisha wasifu wako wa kazi nyinginezo ulizowahi kufanya kabla na hii unayoomba sasa. Bila shaka si mchezo.

Lakini Usijali. Msaada Uko Hapa!

Ni kweli kuandika maombi ya kazi kunahitaji “Ubingwa” wa hali ya juu. Lakini, katika ulimwengu huu ubingwa si kuandika maombi ya kazi tu. Unaweza kuwa bingwa katika mambo mengine. Na wewe ni shahidi kwamba wapo watu wengi ambao hata kusoma au kuandika ni shida lakini ni “Mabingwa” kweli katika nyanja zingine. Kwa hiyo hapa jambo la msingi ni hili: katika dunia hii huwezi kuwa bingwa katika kila kitu. Fundi wa magari akiumwa ataenda kwa daktari kutibiwa. Na daktari akiharibikiwa gari ataenda kwa fundi magari. Kila mmoja wao akitaka ajue vyote basi mwishowe ataishia kuwa hajui lolote. Ndiyo maana sisi kabla hatujakusaidia kukuandikia maombi ya kazi ni lazima tutumie muda wa kutosha kuhojiana na wewe kwanza kupata taarifa zako muhimu na wasifu wako kwa ujumla. Ndipo tutakapoweza kufuma pamoja taarifa hizi katika namna ambayo zitajenga sifa zinazotakiwa na mwajiri wa kazi uliyoilenga wewe.

WALENGWA WA HUDUMA HII NI AKINA NANI?

Kimsingi kila anayetafuta kazi na ambaye angependa kusaidiwa kuandika maombi ni mlengwa wa huduma hii. Unaweza kusema kundi mojawapo ni lile la wale waliohitimu mafunzo mbali (Elimu ya juu ya Vyuo vikuu, Vyuo vya kati, Vyuo vya Ufundi, n.k.). Na kundi lingine ni lile la wengine wote waliosalia.

IN ENGLISH

WE GIVE YOU PROFESSIONAL ADVICE ON HOW TO GET A JOB AT AN AFFORDABLE FEE
NOTE:

It should be very clear this service is NOT free-of-charge. It’s a paid service. However, the good news is that the fee is very affordable.

HOW TO CONTACT US

Look on the right hand column of this advert. You will see the Phone Sign. Click on this Sign and Phone number will appear. Send a short text message to this number asking how much you need to pay for the service. We will respond accordingly.

DISCLAIMER

Read the whole advert carefully in its entirety. It’s written in English and Swahili and whichever language you choose will let you have the intended objective. We are not an Employer or Recruitment Agency. We don’t lobby employers for certain applicants to be employed. We are limited to partnering with the clients/applicants to identify opportunities and collaboratively write Job Application Documents that provide the best chance to be shortlisted for an interview. The client/applicant is solely responsible for final edits, submission to recruitment agency/potential employer, and any claims arising out of or relating to such submission.

PROFESSIONAL WRITING SERVICE

Are you looking for Job? Do you want professional coaching in writing Job Application documents that create a lasting, positive impression? Then, Business Consultancy Services is the right place, and this is the right time.

But first, let's face it: for every advertised Job Position especially in the private sector, employers and recruitment agencies receive a minimum of 1000 application documents from candidates across Tanzania (i.e., 500 Resumes/CVs and 500 Cover Letters). No wonder the selection committee spends no more than 10 seconds to scan and decide whether a particular candidate’s application package goes into “YES” section (meaning will be read later in its entirety) or ends up in a “NO” section (end of story). And while we are still here please note that, at this stage in the recruitment process, you are not physically present. It’s only your application documents which speak on your behalf. Needless to say, it is everyone’s wish that his/her application package demonstrates an edge above the rest of received applications.

It is on this basis, every job application material you submit (cover letter, resume/CV, etc.) must be unique in every way: polished, precise, professional, consistent, and balanced to perfection. It needs to go beyond mere chronological order/list of your experience, skills and employment history. But how is that even possible?

Don’t worry. Help Is Here!

Writing is an Art. But, there are many people in this world who are Geniuses in different areas except for writing. The bottom line is; you can’t be good in everything. And let’s face it, your ignorance in other areas of life is what made you dedicate all the time in that single area where they call you “Genius” or they simply agree that you always do what you do best. At Business Consultancy Services, this truth is not just understood but it’s a way of life. That’s why ample time is spent with you to understand your history, skills, experience, strengths, etc., and how all these can be brought together to produce the right mix of information that will sell you to potential employers in the most effective and appropriate way.

WHO ARE THE TARGET BENEFICIARIES?

Generally, every Job Seeker in Tanzania especially FRESH GRADUATES from Universities, Colleges or other training institutions – VETA, tourism and hospitality industry, etc.