Wasimamizi Wa Ukoboaji (32)

at Karagwe District Cooperative Union ( KDCU LTD )
Location Karagwe, Tanzania, United Republic of
Date Posted May 19, 2020
Category Agriculture
Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
Tangazo La Kazi Za Msimu 2020/2021
Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya KARAGWE na KYERWA (KDCU LTD) kinatarajia kuanza ukusanyaji wa kahawa kwa msimu 2020/2021.
Kama ilivyo kwa misimu yote kuna nafasi za kazi za msimu zinazotakiwa kujazwa kabla ya zoezi la ukusanyaji wa kahawa kuanza. Nafasi hizo ni kama ifuatavyo .

Job Responsibilities: Not Specified

Job Skills: Not Specified

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
• Awe na umri wa miaka 25 na kuendelea
• Awe na uzoefu wa kusimamia kazi viwandani kwa muda wa miaka miwili
• Awe na wadhamini wawili watakaokuwa tayari kumdhamini kwa kutoa mali zao zisizohamishika zenye thamani si chini ya milioni thelathini.
• Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kujituma
• Awe anajua kusoma na kuandika kwa ufasaha.

Applying Instructions

Masharti Ya Jumla Kwa Waombaji
• Awe ni raia wa Tanzania
• Awe na umri wa miaka 18 hadi 40
• Awe na tabia njema ya kuridhisha inayokubaliwa kwenye jamii
• Awe hajawahi kuhukumiwa na kufungwa kwa kosa la jinai.
• Maombi yote yaandikwe kwa mkono na kuambatanisha nakala za vyeti vya shule na taaluma na picha yaani passport size mbili na au nakala (photocopy) ya kadi ya mpiga kura, kitambulisho cha Taifa au kitambulisho chochote
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 23/05/2020 Saa 8:00 Mchana. Maombi yote yatumwe kwa anwani ifuatayo;
Meneja Utumishi/Utawala,
KDCU Ltd, S.L.P 14,
KARAGWE
NB: Waombaji watakaotimiza vigezo watajulishwa kupitia mbao za matangazo tarehe ya usaili.