UTAPELI WA AJIRA ZA ZOOM

at Mriporti wezi wa zoom
Location Dar es Salaam, Tanzania, United Republic of
Date Posted December 30, 2021
Category Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

Description

Habari ndugu zangu mnaotafuta ajira humu Zoom.
Ukweli ni kwamba zoom inarahisisha kupata matangazo ya ajira mbalimbali ila shida inakuja matangazo mengi ya humu yanayohusu ajira ni utapeli hao wanaotangaza na wao wanatafuta ajira yaani hawana kazi ya kukupa

  1. JOB JUNCTION.
    Huyu jamaa yupo makumbusho pale ni declare interest kwamba hata mimi amenipiga pesa yangu.
    Huyu kaja kijanja zaidi hata akanipata na mimi
    Huyu anatangaza kazi humu Zoom tena huwa anatangaza kazi ambazo watu wengi wanazipenda na anaweka uzoefu wa mwaka moja ili anapata wengi
    Kazi zake utasikia
    Bank teller.
    Loan officer
    Sales supervisor
    Office administrator

Na mshahara wake kazi zake zote ni 1,000,000-1,500,000

Huyu jamaa naweza sema mkatiri sana
Ukiomba hizo kazi anawaita pale ofisini kwake makumbusho stand anawambia mimi sina kazi yavkukupa ila ninachofanya mimi nakuunganisha na kampuni ambazo utaenda kufanya interview anakusisitiza kabisa kama huna uwezo wa kufanya interview basi hapo hapakufai
Mwisho anakwambia ila unatakiwa utoe elfu 30 ili kuchangia huduma za ofisi hapa si unajua lengo letu sisi kusaidia vijana
Wewe utamuona kama mtu wa maana na utaona kama ishu ni kufanya interview basi nitaweza mana anakwambia atakuunganisha makampuni mengi sana ndani ya muda wa mwaka
KICHEKESHO CHAKE SASA
Huyu jamaa kweli anakuunganisha na makampuni ila sasa hayo makampuni na hizo kazi zenyewe ndio kituko kwani hizo kazi anazotangaza hapo zoom hazipo kabisaaaa yeye atakuunganisha kwenye kampuni ambazo mshahara wa ni 150000 yaani laki na nusu mwisho laki 3 au laki mbili na nusu yaani hana hata kampuni moja inayoweza kukulipa hata laki nne mimi nimefanya interview zake zaidi ya makampuni 7 ila yote mishahara yao chini ya laki tatu.
Mbaya zaidi asilimia kubwa ya makampuni yake hata ukigugo hayapo yaani vikampuni vya mfukoni.
Na akanitia hasira zaidi akanipeleka kwenye kampuni zingine unalipwa kwa commission sasa unamuuliza mbona unatangaza kazi zingine halafu interview unatupeleka kazi zingine hana jibu
Yaani yeye nae mwizi tu anahitaji zile elf30 zenu tu basi

USHAURI WANGU TUWENI MAKINI SANA NA WANAOTANGAZA AJIRA ZOOM HUMU yapo matangazo ya ukweli ila ya uongo mengi sana
Mi mwenyewe nimepata ajira kwa matangazo ya zoom pia ila baada ya kuliwa elf30 yangu na jobujanction??