Mtunza Stoo/Ghala

at Chawakim Cooperative Society Ltd
Location Dar es salaam, Tanzania, United Republic of
Date Posted January 29, 2020
Category Management
Production / Manufacturing
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
Chawakim Cooperative Society Ltd .

MAJUKUMU YA KAZI
• Kuandaa na kutunza kumbukumbu zote za maziwa yanayoingia na mtiririko wake wote(stock movement)
• Kupokea na kukagua ubora wa maziwa yanayoingia kwa ajili ya uzalishaji
. • Kupitia mara kwa mara mahitaji ya malighafi kulingana na uhitaji wa uzalishaji na kutoa taarifa kwa Meneja ili kuhakikisha uwepo wa malighafi za kutosha
. • Kuandaa na kutunza taarifa za manunuzi ya vifaa na malighafi za uzalishaji
• Kuandaa na kutunza kumbukumbu ya maziwa yaliyopokelewa siku hadi siku.
• Kufanya uhakiki wa maziwa na malighafi nyingine za Chama kwa kushirikiana na Mhasibu kwa ajili ya kufunga hesabu za mwaka.

Job Skills: Not Specified

SIFA ZA MWOMBAJI
• Awe na Stashahada katika fani ya manunuzi,ugavi na uhasibu (Ordinary Diploma in Procurement and Logistic Management/ Material Management and accounting) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
• Awe na umri wa miaka 25 na kuendelea
• Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
. • Awe amefanya kazi kwenye kiwanda cha maziwa.
• Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili (2) katika fani aliyoomba
• Awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai
• Awe na sifa ya uadilifu

Applying Instructions

Job application procedure
MASHARTI YA JUMLA KWA NAFASI YA KAZI
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania
• Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa
• Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika, Barua iliyoandikwa kwa mkono na kusainia.
• Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika, Vyeti vya kitaaluma (Professional Certificate from respective Board)
• “Testmonials” “Provisional Results”, “Statement of results” hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
• Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA, na NACTE)
• Mwombaji atakayeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili
• Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili
• Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
• Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
• Maombi yote yatumwe kupitia anuani tajwa hapa chini
• Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10th February 2020

MWENYEKITI WA BODI
CHAWAKIM COOPERATIVE SOCIETY LTD
S.L.P 30871,
KIBAHA, TANZANIA.
E mail: chawakim@yahoo.com