Msimamizi wa AMCOS (Nafasi 1)

at Duga Agricultural Marketing Co-operative Society LTD (DUGA AMCOS)
Location Tanga, Tanzania, United Republic of
Date Posted November 30, 2021
Category Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

Description

Duga Agricultural Marketing Co-operative Society LTD (DUGA AMCOS).

Chama cha DUGA AMCOS kilichosajiliwa mwaka 2012 chenye usajili nambari TAR 4002 ni muungano wa watu (wakulima) chini ya sheria ya vyama vya ushirika nambari 6 ya mwaka 2013, wanaofanya kazi kwa hiari ili kufanikisha mahitaji yao ya kiuchumi na kijamii kupitia shughuli za biashara inayomilikiwa kwa pamoja (Korosho) na kuthibitiwa kwa uwazi. Chama hiki kinazingatia maadili ya kujisaidia wenyewe, majukumu binafsi, usawa na mshikamano.

Chama hiki kipo kata ya Duga wilayani Mkinga, mkoani Tanga kikiwa na lengo kuu la kuinua na kustawisha hali ya uchumi na maisha ya wanachama kwa kuongeza mapato kupitia uzalishaji wa shughuli za kilimo cha zao la Korosho. Chama hiki kwa kushirikiana na shirika la CARE Tanzania na kampuni ya Out-Growers Aps wanatekeleza mradi wa kuboresha mnyororo wa thamani wa zao la Korosho katika kata tano za wilaya ya Mkinga (Mayomboni, Duga, Sigaya, Moa na Mwakijembe) wenye ufadhili wa DANIDA ambao utatekelezwa kwa muda wa kipindi cha miaka minne kuanzia Julai 2021 hadi Juni 2025. Lengo la mradi huu ni kuchangia ukuaji jumuishi wa kiuchumi na endelevu katika mnyororo wa thamani wa zao la korosho nchini Tanzania kupitia usindikaji wa ndani, uwekezaji wa pamoja na uongezaji wa thamani unaozingatia utunzaji wa mazingira. Ili kutekeleza mradi huu, mwenyekiti wa chama cha Duga AMCOS anarudia kutangaza nafasi za kazi zifuatazo :-

1) Msimamizi wa AMCOS (Nafasi 1)

Majukumu:
i. Kusimamia na kuhakikisha wanachama na viongozi wa AMCOS wanapata mafunzo yote yatakayotolewa na mradi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za mafunzo.
ii. Kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya kuwajengea uwezo Bodi ya chama na wakulima, na kuhakikisha menejimenti ya chama inafuata kanuni na taratibu za mradi na utekelezaji wa biashara kati ya AMCOS na wabia wake (Out-growers Kilimo)

Sifa: Awe na shahada ya Biashara au usimamizi wa ushirika kutoa chuo kinachotambulika na serikali na uzoefu wa kufanya kazi na vyama vya ushirika kwa miaka 3 na kuendelea.