Msambaza Nyaraka za Mahakama

at The United Republic Of Tanzania Court
Location Dar Es Salaam, Tanzania, United Republic of
Date Posted February 12, 2021
Category Government
Legal
Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mahakama ya Tanzania inapenda kuutangazia umma kwamba kuna nafasi za kazi za Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama watakaofanya kazi katika Mikoa mbalimbali Tanzania Bara. Kwa mujibu wa Kanuni ya 4 na ya 6 ya Kanuni za Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama Na. 363 za Mwaka 2017(The Court Brokers and Process Servers (Appointment, Remuneration and Discipline) Rules, GN No. 363 of 2017), Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama pamoja na majukumu mengine, imepewa jukumu la kuteua Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama wenye sifa kama zilivyoainishwa hapa chini. .

Sifa za Waombaji.
• Raia na Mkazi wa Tanzania mwenye umri wa utu uzima.
• Awe ana Leseni au kuwa tayari kujisajili kwa ajili ya kupata Leseni ya kufanya kazi ya Msambaza Nyaraka za Mahakama.

• Awe na Elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea na awe na uwezo wa kuzungumza Kingereza na Kiswahili fasaha.
• Awe amehudhuria mafunzo ya majukumu ya Msambaza Nyaraka za Mahakama yanayotolewa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA) na kutunukiwa Cheti cha Umahiri (Certificate of Competence).
• Awe anafahamu kikamilifu Kanuni za Usambazaji Nyaraka za Mahakama kama zilivyoainishwa na Sheria ya Mwenendo wa Madai na Sheria nyingine husika.
• Awe amelipa ada ya maombi ya kiwango cha Shilingi 30,000/= ambayo haitarejeshwa.

Job Skills: Not Specified

Kazi za kufanya.
Kusambaza nyaraka za Mahakama zinazotokana na mwenendo wa Mashauri na zinazotolewa nje ya mwenendo wa Mashauri ambazo zinajumuisha:-
• Wito wa kuitwa Shaurini, taarifa, nakala za Hukumu, nakala za Maamuzi, tuzo au amri nyingine halali za Mahakama.
• Taarifa ya uteuzi wa Dalali wa Mahakama.
• Nyaraka nyingine zozote zitakazotolewa na Mahakama.

Ada, gharama na posho za Wasambaza Nyaraka za Mahakama.
Ada, gharama na posho atakazolipwa Msambaza Nyaraka za Mahakama ni kama zilivyoainishwa katika Kanuni ya 30 na 31 ya Kanuni za Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 363 la Mwaka 2017 (The Court Brokers and Process Servers (Appointment, Remuneration and Discipline) Rules, GN No. 363 of 2017).
Barua zote za maombi ya Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama zitumwe kwa Katibu wa Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama kupitia kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi (Mkoa) ambapo ndio Mkoa ambao Dalali wa Mahakama au Msambaza Nyaraka za Mahakama anaotarajia kufanyia kazi. Aidha, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi (Mkoa) ana wajibu wa kuwasilisha taarifa ya siri ya Mwombaji kazi ya Udalali wa Mahakama na Usambazaji Nyaraka za Mahakama kwa Msajili, Mahakama Kuu ya Tanzania.

Barua ya maombi ya Usambazaji Nyaraka za Mahakama iambatanishwe na:-
• Kivuli cha Cheti cha Elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea.
• Kivuli cha Cheti cha Umahiri (Certificate of Competence) cha majukumu ya Msambaza Nyaraka za Mahakama kilichotolewa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA).
• Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV). (Taarifa isiwe na “Referees” ambaye ni ndugu, jamaa au rafiki mwenye uhusiano wa karibu na mwombaji).
• Kivuli cha Cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha Uraia.
• Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
• Fomu ya Maombi ya Msambaza Nyaraka za Mahakama (Fomu Na. 4) iliyojazwa kikamilifu.
• Leseni ya Biashara kutoka katika Halmashauri ya Jiji, Mji au Manispaa au ahadi ya kuwa tayari kukata Leseni hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Msambaza Nyaraka za Mahakama.
• Barua ya utambulisho juu ya tabia ya Mwombaji kutoka kwa watu wanaoaminiwa. (Barua isiandikwe na ndugu, jamaa au rafiki mwenye uhusiano wa karibu na mwombaji).
• Fomu ya Wadhamini wawili wa Muombaji (Fomu Na. 5) yenye jumla kiwango cha udhamini kisichopungua Milioni mia nne (400,000,000/=).
• Nakala ya uthibitisho wa malipo ya Kodi(TIN).
• Hati ya kubadilisha jina (Deed Poll) iwapo kuna tofauti ya majina katika nyaraka zitakazotumika katika maombi ya Mwombaji.

Applying Instructions

Fomu zote za maombi ya Udalali wa Mahakama na Wadhamini wake na Wasambaza Nyaraka za Mahakama zinapatikana katika Ofisi zote za Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi (Mkoa) Tanzania Bara na Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19/02/2021 saa 9:30 alasiri.
Mwombaji wa nafasi ya Dalali wa Mahakama na Msambaza Nyaraka za Mahakama aandaye nakala tatu (3) na atume maombi yake kwa njia ya Posta (E.M.S) au kwa Mkono na kuwasilishwa kwa Msajili, Mahakama Kuu, S.L.P 9004, DAR ES SALAAM.
na:-
M.J. Chaba
Kny: MSAJILI
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA