Machine Operator/FUNDI MITAMBO

at Chawakim Cooperative Society Ltd
Location Dar es salaam, Tanzania, United Republic of
Date Posted February 26, 2020
Category Engineering
Production / Manufacturing
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

Job Summary

Chama kinatafuta Machine Operator/fundi mitambo wa mashine za kuhifadhi za kuzalisha maziwa.

  • Minimum Qualification: Unspecified
  • Experience Level: Mid level
  • Experience Length: 3 years

Job Description

MAJUKUMU YA KAZI

a) Atafanya usafi wa jumla wa mashine(CIP) kwa muda usiopungua nusu saa

b) Kuangalia hali ya mashine kabla ya uzalishaji kwa mfano kuangalia Oil,kutoa unyevu kwenye compresa, kuangalia uzima wa heater na pump, kuangalia mfumo wa umeme kama upo sawa.

c) Kuhakikishwa vyombo vyote vimesafishwa kwa maji ya moto yaliyochemka.

d) Kuhakikisha kuwa kwenye mashine hakuna sehemu inayovuja maji au maziwa

e) Awe na uzoefu wa kwenye kiwanda cha maziwa kwa miaka 3.

f) Kufanya service ya mashine kulingana na ratiba

g) Kushirikiana kwa karibu na afisa uzalishaji ili kuhakikisha kuwa bidhaa inayozalishwa inakidhi viwango.

SIFA ZA MACHINE OPERATOR

a) Awe na elimu ya O’level

b) Awe na mafunzo ya VETA katika fani ya umeme/Refrigiration

c) Awe na uzoefu wa kiwanda cha maziwa usiopungua miaka 3.

d) Awe mwaminifu na mwadilifu

e) Mchapakazi na anayejituma

f) Awe tayari kufanya kazi wakati wowote atakapohitajika

g) Awe na ushirikiano na wafanyakazi wenzake

MSHAHARA

Kiwango cha mshahara (…………….ni makubaliano)

MASHARTI YA JUMLA KWA NAFASI ZOTE ZA KAZI

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania

ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa

iii. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika, Barua iliyoandikwa kwa mkono na kusainia.

iv. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika, Vyeti vya kitaaluma (Professional Certificate from respective Board)

v. “Testmonials” “Provisional Results”, “Statement of results” hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA

vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA, na NACTE)

vii. Mwombaji atakayeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili

viii. Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili

ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

x. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

xi. Maombi yote yatumwe kupitia anuani tajwa hapa chini

Applying Instructions

MWENYEKITI WA BODI

CHAWAKIM COOPERATIVE SOCIETY LTD

S.L.P 30871,

KIBAHA TANZANIA

E mail: chawakim@yahoo.com