Kubeba Magunia Ya Kahawa (100)

at Karagwe District Cooperative Union ( KDCU LTD )
Location Karagwe, Tanzania, United Republic of
Date Posted May 19, 2020
Category Agriculture
Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
Tangazo La Kazi Za Msimu 2020/2021
Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya KARAGWE na KYERWA (KDCU LTD) kinatarajia kuanza ukusanyaji wa kahawa kwa msimu 2020/2021.
Kama ilivyo kwa misimu yote kuna nafasi za kazi za msimu zinazotakiwa kujazwa kabla ya zoezi la ukusanyaji wa kahawa kuanza. Nafasi hizo ni kama ifuatavyo .

Job Responsibilities: Not Specified

Job Skills: Not Specified

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
• Awe na umri wa miaka 18 na kuendelea
• Awe tayari kufanya kazi kwa kiwango cha malipo kitakachopangwa na KDCU Ltd
• Mwombaji afahamu kwamba KDCU Ltd haitaongeza kiwango cha malipo mpaka mwisho wa msimu (d) Awe tayari kufanya kazi yoyote atakayopangiwa na msimamizi wake wa kazi
• Afahamu kuwa hataruhusiwa kuja kazini akiwa amelewa au kunywa pombe wakati wa kazi
• Awe tayari kufanya kazi kwa kuzingatia maelekezo anayopewa na uongozi
• Afahamu kwamba ni marufuku kupigana wakati wa kazi
• Afahamu kwamba ni marufuku kutumia lugha ya matusi akiwa kazini
• Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kujituma

Applying Instructions

Masharti Ya Jumla Kwa Waombaji
• Awe ni raia wa Tanzania
• Awe na umri wa miaka 18 hadi 40
• Awe na tabia njema ya kuridhisha inayokubaliwa kwenye jamii
• Awe hajawahi kuhukumiwa na kufungwa kwa kosa la jinai.
• Maombi yote yaandikwe kwa mkono na kuambatanisha nakala za vyeti vya shule na taaluma na picha yaani passport size mbili na au nakala (photocopy) ya kadi ya mpiga kura, kitambulisho cha Taifa au kitambulisho chochote
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 23/05/2020 Saa 8:00 Mchana. Maombi yote yatumwe kwa anwani ifuatayo;
Meneja Utumishi/Utawala,
KDCU Ltd, S.L.P 14,
KARAGWE
NB: Waombaji watakaotimiza vigezo watajulishwa kupitia mbao za matangazo tarehe ya usaili.