Katibu Mahsusi III

at Arusha City Council
Location Arusha, Tanzania, United Republic of
Date Posted December 17, 2020
Category Government
Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Jiji la Arusha kutuma maombi ya kazi ya muda kwa Mkurugenzi wa Jiji ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya Tangazo hili. Nafasi hizi ni za muda wa miezi sita kwa kazi zilizopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021. .

Sifa zinazotakiwa
Awe na elimu ya Kidato cha nne aliyehudhuria mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu.Awe amefaulu somo la hatimkato ya Kiswahili na kiingereza maneno themanini kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya compyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali na kupata cheti katika program za windows Microsoft office Internet, E-mail na Publisher.

Job Skills: Not Specified

Kazi na Majukumu
• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zoa na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
• Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anapofanyia kazi na kumuarifu mkuu wake kwa wakati unaohitajika
• Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.

Applying Instructions

MAELEZO YA JUMLA
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na Mwenye akili timamu.
• Waombaji wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
• Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu/taaluma, cheti cha kuzaliwa na maelezo binafsi (CV).
• Mshahara utakuwa wa makubaliano kwa kuzingatia bajeti.

• Maombi yatakayotumwa kwa mkono hayatapokelewa.
• Waombaji wenye uzoefu wa kazi watapewa kipaumbele.

Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Jiji la Arusha
S.L.P. 3013, Arusha.