Katibu Mahsusi Daraja III TGS B (6)

at Judiciary of Tanzania
Location Dar es salaam, Tanzania, United Republic of
Date Posted May 7, 2020
Category Legal
Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

Overview

The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 vests the authority and responsibility to administer justice in the Judiciary of Tanzania. The Judiciary has its foundation on Article 107A (1) and 107B of the Constitution and states clearly about the Independence of the Judiciary in the United Republic of Tanzania. Now the strategic plan for Judicial Independence is focused in both form and content.


1:2 Mandate of Judiciary
The mandate of Judiciary to perform its functions is obtained from the Constitution of the United Republic of Tanzania vide article 107 and its primary function is to dispense justice with equity and compassion according to laws of Tanzania.
JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
UMOJA NA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 195
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine, mamlaka ya kuajiri watumishi wa Mahakama wa kada mbalimbali.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania kwenye Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi..

Kazi za kufanya:
• Kufanya kazi Typing pool’au chini ya Katibu Mahsusi mwingine mwenye cheo cha juu kumzidi kwenye ofisi ya Mkuu wa sehemu au kitengo.
• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanazoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa, kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
• Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika kwa shughuli za kazi hapo ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wa kazi kwa
• wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa
• walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

Job Skills: Not Specified

Sifa za kuingilia:
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Uhazili Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza (Shorthand) maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher

Applying Instructions

Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 21/05/2020 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:

  •  Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo. - Wasifu wa mwombaji (CV).
  • Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  • Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni ambazo zimeandikwa majina nyuma yake .
  • NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/ sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).

Aidha, inasisitizwa kwamba:

  •  Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44
  • Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa Wilaya anayoishi mwombaji.
  •  Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.
  •  Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
  •  Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
  •  Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.
  • Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
  • Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.
  •  Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.
  •  Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.
  •  Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391, DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;
Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391, DAR ES SALAAM,