DriverWalinzi (3)

at Rijk Zwaan
Location Arusha, Tanzania, United Republic of
Date Posted May 20, 2020
Category Security
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

Job Summary

Kulinda mali za kampuni, mazingira yanayozunguka kampuni na nyumba za wafanyakazi wenye stahiki ya kupewa walinzi majumbani. Kuelewa na kushiriki katika kudhibiti matukio mbalimbali yanayohusiana na majanga ya asili kama vile mafuriko na matukio yanayoweza kuleta madhara kwa wafanyakazi au mali za kampuni. Mlinzi atakua chini ya kitengo cha Stesheni na ataripoti kwa Mratibu wa walinzi.

  • Minimum Qualification: Highschool
  • Experience Level: Entry level
  • Experience Length: 2 years

Job Description

Majukumu:

1. Kufika eneo la kazi kwa wakati na kufanya makabidhiano ya lindo kwa usahihi.

2. Kufika eneo la kazi kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa.

3. Kuzingatia sera ya ulinzi, protokali na miongozo iliyowekwa na kampuni.

4. Kuhakikisha usalama wa wafanyakazi, wageni na mazingira ya kampuni.

5. Kuripoti kwa mratibu wa walinzi (Security Team Coordinator) matukio yote, ajali au dharura zinazojitokeza mazingira husika ya kazi.

6. Kuandaa na kupokea muhtasari wa ripoti ya matukio kabla na baada ya kazi.

Sifa za Mwombaji:

  • Uwezo wa kufanya kazi vizuri na timu.
  • Kuielewa vizuri shughuli za kampuni hii.
  • Awe na uwezo wa kuandika ripoti
  • Uwezo wa kufanya kazi katika taasisi ya kimataifa.
  • Uelewa mzuri wa lugha ya Kiswahili kwa kusoma na kuandika
  • Uelewa wa lugha ya Kiingereza ni kigezo cha nyongeza.
  • Kufanya kazi kwa kufuata taratibu na kuhudumia wateja wa kampuni.
  • Uwezo wa Kujitegemea na kuwasiliana vizuri.
  • Mwaminifu.
  • Awe mkazi wa Arusha

Elimu na Uzoefu:

  • Elimu ya Sekondari
  • Aliyepitia mafunzo ya mgambo
  • Awe na uzoefu wa miaka miwili (2)

Applying Instructions

Please send your CV and your motivation to

  ajira@rijkzwaan.com

Only short- listed candidates will be contacted.

Or You can send your application to

Human resource Manager,

 Rijk Zwaan Q-Sem Ltd

 P.o Box 12345

 Arusha.