AFISA MASOKO (4)
Location | Dar es Salaam, Tanzania, United Republic of |
Date Posted | May 19, 2022 |
Category | Management |
Job Type | Full-time |
Currency | TZS |
Description
Description
NAFASI : AFISA MAUZO NA MASOKO
MAJUKUMU
- Kutangaza na kutafuta wateja wa kununua viwanja vilivyopimwa kwenye miradi iliyopo katika miji ya Tanga, Dar es Salaam, Morogoro na sehemu nyingine kadiri itakavyopangwa na utawala.
- Kuwaongoza wateja katika zoezi la kutembelea miradi ya viwanja pamoja na kuwaonyesha viwanja vilivyopo sokoni.
- Kumwelezea mteja mambo mbalimbali na masharti yaliyo katika mikataba ya mauziano ya viwanja
- Kuishauri kampuni namna bora ya kufanya matangazo ili kukuza kipato cha kampuni.
- Kufanya utafiti juu ya maeneo mapya ya masoko
- Kujenga taswira nzuri ya kampuni kwa wateja
VIGEZO - Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi
- Awe mwaminifu, mchangamfu na mwenye ushawishi kwa wateja
- Awe na angalau elimu ya Kidato cha Nne au zaidi
- Awe na simu ya kisasa (smartphone)
- Awe na uelewa walau kidogo wa matumizi ya Computer na simu za kisasa
- Ajue kusoma, kuandika na kuhesabu vizuri Kiswahili, kufahamu Kiingereza kunampa nafasi ya juu mwombaji