6 Dereva II (magari)

at Arusha City Council
Location Arusha, Tanzania, United Republic of
Date Posted December 17, 2020
Category Government
Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Jiji la Arusha kutuma maombi ya kazi ya muda kwa Mkurugenzi wa Jiji ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya Tangazo hili. Nafasi hizi ni za muda wa miezi sita kwa kazi zilizopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021. .

Sifa zinazotakiwa
Awe na Elimu ya kidato cha nne na Leseni ya daraja E au C1 ya uendeshaji wa magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha mafunzo ya ufundi stadi(VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali.

Job Skills: Not Specified

Kazi na Majukumu
• Kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali na usalama wa gari.
• Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
• Kufanya usafi wa gari
• Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
• Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.

Applying Instructions

MAELEZO YA JUMLA
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na Mwenye akili timamu.
• Waombaji wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
• Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu/taaluma, cheti cha kuzaliwa na maelezo binafsi (CV).
• Mshahara utakuwa wa makubaliano kwa kuzingatia bajeti.

• Maombi yatakayotumwa kwa mkono hayatapokelewa.
• Waombaji wenye uzoefu wa kazi watapewa kipaumbele.

Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Jiji la Arusha
S.L.P. 3013, Arusha.