38 Wafanya usafi (Utawala 3, Mazingira 34 na Kilimo1)

at Arusha City Council
Location Arusha, Tanzania, United Republic of
Date Posted December 17, 2020
Category Government
Management
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Jiji la Arusha kutuma maombi ya kazi ya muda kwa Mkurugenzi wa Jiji ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya Tangazo hili. Nafasi hizi ni za muda wa miezi sita kwa kazi zilizopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021. .

Sifa zinazotakiwa
Awe na elimu ya Kidato cha nne.

Job Skills: Not Specified

Kazi na Majukumu
Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ya ofisi ikiwa ni pamoja na kufagia kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo na kufanya usafi maeneo mbalimbali ya Mji.

Applying Instructions

MAELEZO YA JUMLA
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na Mwenye akili timamu.
• Waombaji wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
• Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu/taaluma, cheti cha kuzaliwa na maelezo binafsi (CV).
• Mshahara utakuwa wa makubaliano kwa kuzingatia bajeti.

• Maombi yatakayotumwa kwa mkono hayatapokelewa.
• Waombaji wenye uzoefu wa kazi watapewa kipaumbele.

Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Jiji la Arusha
S.L.P. 3013, Arusha.