25 Msaidiziwa HesabuI (Accounts AssistantI)

at Arusha City Council
Location Arusha, Tanzania, United Republic of
Date Posted December 17, 2020
Category Accounting
Audit
Finance
Government
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Jiji la Arusha kutuma maombi ya kazi ya muda kwa Mkurugenzi wa Jiji ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya Tangazo hili. Nafasi hizi ni za muda wa miezi sita kwa kazi zilizopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021. .

Kazi na Majukumu
ya Msaidizi wa Hesabu I(Accounts Assistant I): • Kutunza daftari la fedha la matumizi ya kawaida na maendeleo.
• Kutunza nyaraka za hati za malipo.
• Kuingiza mapato na matumizi kwenye vutabu vya fedha
• Kuandika taarifa za mapato mbalimbali za fedha zilizopokelewa.
• Kufanya kazi zingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake.

Job Skills: Not Specified

Sifa zinazotakiwa
Awe na Stashahada ya uhasibu kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali au mwenye cheti cha ATEC II inayotolewa na NBAA au sifa inayolingana na hizo inayotambulika na NBAA

Applying Instructions

MAELEZO YA JUMLA
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na Mwenye akili timamu.
• Waombaji wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
• Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu/taaluma, cheti cha kuzaliwa na maelezo binafsi (CV).
• Mshahara utakuwa wa makubaliano kwa kuzingatia bajeti.

• Maombi yatakayotumwa kwa mkono hayatapokelewa.
• Waombaji wenye uzoefu wa kazi watapewa kipaumbele.

Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Jiji la Arusha
S.L.P. 3013, Arusha.