25 Askari polisi wasaidizi (Auxiliary police)

at Arusha City Council
Location Arusha, Tanzania, United Republic of
Date Posted December 17, 2020
Category Security
Government
Job Type Full-time
Currency TZS

Description

JOB DETAILS:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Jiji la Arusha kutuma maombi ya kazi ya muda kwa Mkurugenzi wa Jiji ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya Tangazo hili. Nafasi hizi ni za muda wa miezi sita kwa kazi zilizopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021. .

Kazi na Majukumu
• Kulinda na kudumisha usalama wa Halmashauri na mali zake.
• Kulinda watu na mali zao katika eneo la Halmashauri.
• Kusimamia utekelezaji wa sheria kanuni na taratibu zilizopo.
• Kufanya doria maeneo mbalimbali ya Halmashauri.
• Kutuliza fujo inapotokea tukio linaloashiria uvunjifu wa amani katika eneo la halmashauri.
• Kushiriki kazi za misako katika Halmashauri.
• Kushiriki katika matukio ya dharura pindi yanapojitokeza.
• Kulinda misafara ya viongozi wanapotembea maeneo ya Halmashauri.

Job Skills: Not Specified

Sifa zinazotakiwa
Awe ni raia wa Tanzania mwenye afya njema kiakili na kimwili mwenye macho ya kuona vizuri bila kutumia miwani kwa kiwango cha 6/6r-6/61 mwenye tabia njema asiye na kumbukumbu za kupatikana na hatia ya makosa ya jinai, awe na uwezo wa kusoma na kuandika kiswahili na kingereza na mwenye elimu na ufaulu wa kidato cha nne na stashahada kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.

Applying Instructions

MAELEZO YA JUMLA
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na Mwenye akili timamu.
• Waombaji wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
• Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu/taaluma, cheti cha kuzaliwa na maelezo binafsi (CV).
• Mshahara utakuwa wa makubaliano kwa kuzingatia bajeti.

• Maombi yatakayotumwa kwa mkono hayatapokelewa.
• Waombaji wenye uzoefu wa kazi watapewa kipaumbele.

Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Jiji la Arusha
S.L.P. 3013, Arusha.